Welcome to TANDEN information portal. Thursday, 9th Sep,2010
Username: Password:
Upcoming Tanzanians' events
Tomorrow - Jagwa Music Concert
11 Sep - Eid el Fitri Celebration
18 Sep - TANDEN family day
Public holidays in Denmark
24 Dec - Christmas Eve
25 Dec - Christmas Day
26 Dec - Boxing Day
Denmark: Best African Achievement Awards 2010 ■■ Press release: Mzungu Kichaa on European tour in August 2010 ■■ Dulla Mnanga Album "Nani" is out ■■ Invest in Tanzania■■ Welcome to Tanzania, the land of Kilimanjaro,Zanzibar and Serengeti
Watanzania kasumba hii itaisha lini?

Posted by: Henrype on 21st Nov,2009

MWANADAMU yeyote ana hali ya kujipenda akihitaji kutambuliwa na wenzake kuwa yeye naye yumo na hakika hupendeza. Lakini kwa nini kumezuka mtindo wa watu weusi kutamani kufanya juhudi kubwa ili wafanane na Wazungu kwa rangi ndipo wajisikie wamependeza.

Bila shaka wengi wetu wana majibu tofauti na hata wengi kutokuwa na majibu bali kuchanganyikiwa na kuendelea kuamini kwamba kila kitu au jambo lolote litokanalo na mzungu ndilo jema kuliko yale yenye asili ya mtu mweusi.

Tujifunze kitu ili ikiwezekana tujikwamue kwenye mawazo mgando na kasumba ya kumlaumu Mungu kwanini alituumba watu weusi.

Historia ya mwanadamu kwa mujibu wa maandiko matakatifu inabainisha kuwa Mwenyezi Mungu aliumba mwanaume na mwanamke akiwa ameanza na mwanaume, ndipo katika utaratibu wake akasema hataumba tena kwa mavumbi bali kupitia viungo vya hawa wawili. Jambo ambalo halijulikani wazi ni lile la kusema kama Adamu na Hawa walikuwa na rangi gani kati ya hii ya Kizungu au ya Kiafrika.

Historia inazidi kueleza kwamba wanadamu walipokuwa wanaongezeka katika nchi wakaamua kukusanyika katikati ya dunia na kuamua kujenga mnara mrefu wa kuwafikisha juu alipo Mungu, jambo lililokuwa chukizo kwake.

Kumbuka kuwa watu hawa walikuwa wa namna moja hata wakizungumza lugha moja, lakini Mungu akavunja ule mnara na kuwapatia lugha mbalimbali na hili lilisababisha wasielewane tena katika mawasiliano. Na inaaminika kuwa hapa ndipo chimbuko la tofauti ya lugha za wanadamu.

Maandiko ya kale yanafafanua kuwa siku moja baada ya dunia yote kugharikishwa kwa maji na umati wa watu kuangamia watu wanane tu waliokoka kwa kutumia boti iliyojengwa na mcha Mungu mmoja.

Kundi hili dogo lilikuwa na baba, mama na vijana watatu waliokuwa na wake zao. Inasemekana kwamba watoto wale watatu mmoja ndiye chimbuko la Waafrika, mwingine Mzungu na mmoja muasia wa Mashariki.

Kutokana na tabia zao mbele ya wazazi wao ndivyo mzee wao alivyowabariki kila mmoja kwa kiasi tofauti na mwingine. Na hivyo hata leo tunashuhudia tofauti za uelewa na utendaji wa watu wa makundi ya watu hawa.

Awali watu wa makundi haya matatu walionekana kila mmoja kujivunia na kuona fahari ya kuwa vile alivyo, lakini walivyotawanyika duniani kama agizo la Mungu lilivyowaamuru kundi moja likatamani rasilimali za kundi jingine na kufanya hila na hata kuadaa wengine.

Hawa ni Wazungu waliotamani nchi na mabara ya wenzao hususan bara la Afrika, ambalo bahati njema linaonekana kubarikiwa kwa ardhi yenye rutuba na iliyosheheni madini mengi na kuzungukwa na maziwa, mito na bahari. Huu ndiyo uliokuwa mwanzo wa biashara ya utumwa na mfumo wa nchi nyingine kutawala nchi nyingine yaani ukoloni.

Kwa Tanzania hali si tofauti sana na nchi zingine za bara la Afrika zilizowahi kutawaliwa na Wazungu na kufundishwa kujidharau wenyewe ili wathamini hali na maisha ya Wazungu.

Baada ya Wazungu kufanikiwa kuzikolonisha nchi za Kiafrika walijaribu kuwaaminisha Waafrika kuwa mila na desturi zote za Kiafrika si nzuri na ziko kinyume na mapenzi ya Muumba.

Miongoni mwa vitu walivyotushawishi tuviache ni nyimbo na ngoma zetu za asili na kisha wakatufundisha namna ya kuimba nyimbo za kwao pamoja na kutumia ala za huko kwao.

Hata katika mashule waliyotufundishia kuandika na kusoma walitaka tujitahidi kujua lugha ya kwao ili kurahisisha mawasiliano wakati wanapotutumikisha katika kazi zao.

Ni kipindi hiki ambapo tulilazimika kuitikia kwa maneno ya utwana, yaani ‘ndiyo bwana mkubwa.’ Polepole Watanzania waliwaelewa Wazungu kuwa si watu wa kawaida hivyo kadri muda ulivyokwenda ndivyo tulivyotamani hata watoto wetu wasome ili wajue lugha ya Kizungu na waishi kama Wazungu.

Ijapokuwa wanasiasa wazalendo walijaribu kutushawishi tuipende lugha yetu hata wakaanzisha mitaala ya Kiswahili, lakini tunaona leo tunajiaminisha kuwa Kiswahili hakifai kufundishia vyuoni.

Inasikitisha kuona Watanzania wakitamani si kufanana tu bali kuwa Wazungu kwa rangi, nywele, lugha na mwonekano mzima kati ya wengine.

Inashangaza vile hata wasomi wetu wanavyoshindwa kuepuka kasumba hii ya kujuta na kulaani ni kwa nini Mungu amewaumba kuwa Watanzania weusi hata kufanya juhudi ya kujichubua ngozi kwa kutumia kemikali zinazotengenezwa na Wazungu.

Kwa kujua kwamba tunatofautiana na Wazungu katika rangi, nywele na lugha ndipo wengi hununua nywele bandia zifananazo na nywele za Wazungu na kuvaa kichwani.

Na baada ya Wazungu kuthibitisha kuwapo kwa soko la wajinga, maana wajinga ndiyo waliwao, sasa wamefanikiwa kutengeneza kemikali za kila namna za kupaka au kunywa zinazoweza kubadili nywele na ngozi ya mtu na kuwa kama ya Mzungu.

Jambo hili linasikitisha na kushangaza kwani wataalamu wanasema kemikali hizi si salama kwa afya asilia ya mwanadamu.

Wataalamu hawa wanasema yapo madhara mengi yanayotokana na kujibadilisha uasili wetu ndiyo maana wao hata siku moja pamoja na kutuonea wivu na kutamani yetu, hawathubutu kutamani wajibadilishe kuwa na ngozi au nywele kama za kwetu ijapokuwa hilo kitaalaam linawezekana.

Mwanzoni Watanzania wa jinsia ya kike ndiyo waliokuwa wameathiriwa na kasumba hii, lakini leo tunashuhudia uvunjifu zaidi wa maadili yetu kwa kuwaona wanaume nao wakijichubua ngozi na kubadili nywele zao.

Mtindo huu unashangaza hasa kwa kuwa hata wale wasomi wetu hawaoni shida hii kwamba itafikia mahali athari zake zikaliangamiza taifa letu.

Watanzania tunapaswa kuamini kuwa Mungu alivyotuumba ndiyo mpango wake na kwa kweli tuwazuri na tunapendeza tukijitunza kwa usafi wa mwili na mavazi.

Najua zipo dini zinazochukizwa na jambo hili la kumsahihisha Mungu kwa kazi yake ya uumbaji lakini ajabu baadhi ya viongozi katika kaya au familia zao jamii zinaonekana kufurahia na kutetea tabia hii.

Wito wangu kwa Watanzania na waumini wa dini mbalimbali kujifunza zaidi maandiko tuone vile Mungu anavyopendezwa au anavyochukizwa na teknolojia ya kujibadilisha maumbile yetu asilia.


Comments
On 25th Nov,2009 chafu wrote
Huku manamke ana muoa mwanamke na mwanaume anamuoa mwanaume nini mkolongo mwenzetu kwa mashahili kiboko sana.
On 25th Jan,2010 Mtu wrote
Mbona hamtangazi kifo cha mtanzania mwenzenu Rose Mwajasho
Enter your comment below:
Your Name:

Your Comment:


Enter the security code below
d6pg

Kweli tutafika
Je kashfa hii ni ya kweli ama uzushi?
Salaam Kwa Mh. Edward Lowasa Na Wenzake
TWENDE MBELE
ANTIVIRUS MWAKA 2008
Mifuko ya hifadhi ya jamii mzimu unaouwamaliza Watanzania
Cancer Update from Johns Hopkins
John Mashaka on fake and substandard goods
utapeli sampuli mpya bongo??