Welcome to TANDEN information portal. Thursday, 9th Sep,2010
Username: Password:
Upcoming Tanzanians' events
Tomorrow - Jagwa Music Concert
11 Sep - Eid el Fitri Celebration
18 Sep - TANDEN family day
Public holidays in Denmark
24 Dec - Christmas Eve
25 Dec - Christmas Day
26 Dec - Boxing Day
Denmark: Best African Achievement Awards 2010 ■■ Press release: Mzungu Kichaa on European tour in August 2010 ■■ Dulla Mnanga Album "Nani" is out ■■ Invest in Tanzania■■ Welcome to Tanzania, the land of Kilimanjaro,Zanzibar and Serengeti
BoT yatumia Sh1bilioni kukarabati nyumba ya Gavana Ndulu
Bookmark and Share

Source : Mwananchi
Posted by: Webmaster on 22-Dec-2009

WAKATI tuhuma za matumizi mabaya ya Sh1.4 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za Tanesco zikiendelea kuchunguzwa, Benki Kuu (BoT) inadaiwa kutumia Sh1 bilioni kukarabati nyumba moja ya gavana wake, Profesa Benno Ndulu, Mwananchi imeelezwa.


Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa taasisi hiyo ya fedha imetumia kiasi hicho kukarabati nyumba ya gavana katika mradi wa ukarabati wa nyumba za vigogo wake wanne ambao ni gavana na manaibu wake watatu.


Kwa mujibu wa habari hizo, nyumba iliyokarabatiwa kwa fedha hizo iko Oysterbay eneo la Morogoro Stores, jirani na nyumbani kwa katibu mkuu wa mstaafu wa CCM, Philip Mang'ula jijini Dar es Salaam.


Uchunguzi wa gazeti hili umebaini pia kwamba kigogo anayestahili kuishi kwenye nyumba hiyo (gavana), tayari amehamia na kuishi humo tangu Desemba Mosi mwaka huu.


Hata hivyo, habari zaidi za kiuchunguzi zinabainisha kuwa ukarabati wa nyumba hiyo umetumia gharama mara mbili zaidi ya bei ya kununulia nyumba hiyo. Nyumba hiyo ilinunuliwa kwa dola 400,000 za Kimarekani ambazo ni sawa na takriban Sh500 milioni.


Mbali na nyumba hiyo, nyumba nyingine zinazodaiwa kutafuna fedha za walipa kodi katika ukarabati wake ni ya naibu gavana wa kwanza, Juma Reli iliyo Masaki, Mtaa wa Chole. Nyumba hiyo ilikuwa ikitumiwa na gavana wa zamani, Dk Daud Balali.


Habari zaidi zinadai kuwa Reli alihamia kwenye nyumba hiyo baada ya Gavana Ndulu kuikataa kwa madai kuwa haina bwawa la kuogelea (swimming-pool).


Nyumba nyingine iliyo kwenye tuhuma hizo za kashfa ya ufujaji mamilioni ya walipa kodi ni ile inayotumiwa na naibu gavana wa pili (Bukuku), iliyo Oysterbay pamoja na ya naibu gavana wa tatu (Makila) iliyo Masaki.


Afisa uhusiano wa BoT, Emmanuel Mwero, alipotafutwa na Mwananchi kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo jana, hakutaka kujibu moja kwa moja na badala yake aliweka urasimu wa kutaka maswali yaandikwe kwenye karatasi iliyo na nembo ya gazeti hili ndpo aandae majibu.


"Ahh, kwa hilo, wewe lete maswali yako kwenye 'headed paper (barua yenye nembo)' ya Mwananchi hata leo (jana) au kesho (Leo) utajibiwa kiofisi," alisema Mwero.


BoT ni taasisi ya pili kutuhumiwa kuhusika na ufisadi huo katika mradi wa ukarabati wa nyumba za vigogo wake ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.


Tayari Tanesco imekumbwa na tuhuma kama hizo ambazo bado hazijapoa. Wizara ya Nishati na Madini imeeleza kuwa inaendelea kuzifanyia kazi.


Hata hivyo, tuhuma za ufisadi ndani ya BoT zinadaiwa kuwa kubwa na za kutisha ikilinganishwa na kiwango cha pesa kinachodaiwa kutumika kwa ukarabati kwa nyumba za Tanesco.


Wakati Tanesco inatuhumiwa kutumia Sh.1.4bilioni kwa ajili ya ukarabati wa nyumba saba za vigogo wake, taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa BOT imetumia zaidi ya Sh1bilioni kukarabati nyumba moja, kati ya nyumba nne zilizokuwa katika mradi huo wa ukarabati.


Kiasi hicho cha fedha unaweza kununua nyumba mbili mpya nje ya maeneo ya Jiji la London, Uingereza. Kwa sasa bei ya nyumba katika maeneo ya Cardiff ni Sh450milioni kwa nyumba moja.

Comments
On 23rd Dec,2009 Msinjili D.Remmy wrote
Hapa ndipo wawezakuona jinsi Taifa linapo jipeleka katika machafuko na wmishowe vita bila watu kujua.
Haya yaweza kutokea tena kirahisi sana kwani mkusanyiko na mlundikano wa maovu haya tena yanayofanana umezidi kushamili siku hadi siku. Kumnyonga mtu ama kumpiga mtu risasi hadhalani ni jambo rahisi sana ikiwa kuna sheria inayoruhusu kufanyika jambo hili. Na hii ndiyo njia pekee ya suruhisho ya haya yote, kwani isipotungwa sheria ya kuruhusu unyama huu ufanyike kwa yeyote atakaye fanya ama kujaribu kufanya haya na yale yote ambayo yanawaweka ama kuwapeleka Watanzania katika umasikini mkubwa, Kwa hakika ubadhilifu huu wa fedha za walipa kodi hautakwisha kamwe. Wahenga walsema {mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni} Watanzania wenzangu, hebu tujaribu kugeuza msemo huu na kuwaweka wao kwenye kitanzi ama tuwapige risasi ili familia zao ambazo sasa zinafaidi jasho letu, waonje uchungu wa jasho letu tena kwa aibu. {Bunge ni watanzania halisi {tujitungie sheria kupitia chombo hiki}. Na sheria husika iwatie hatiani hata wale waliofanya ubadhilifu huu hata kabla ya sheria kutungwa. Thanks Much. {Pakistani}
On 23rd Dec,2009 Nyota wrote
This fellow carries the most prestigious title of "Dr.", I think. Just see what any tanzanian can do, worst, a tanzanian with education.
But on the other hand he is sitting on real gold so why not.
On 2nd Jan,2010 Json wrote
Minafikiri ingifika kipindi tukawa wakweli wa mambo hasa yahusuyo maadili ya uongozi nafikiri kipegelehichi cha maadili ya uongozi wa umma hakifanyiwi kazi vilivyo hayo ni ya BOT yameibuka na hii ni kwasababu kashfa ya Epa haijaisha na watuhumiwa bado wako mahakamani na wengine hawajakamatwa bado.Vipi sekta nyengine? Kama vile sekta ya madini na utalii ni mabilioni mangapi watanzania tunapoteza? Jamani amkeni nyie watanzania kwa nini mmekufaaaaa? Mngekuwa mme lala mngestuka toka usingizini!
Mungu amlaze mahali pema peponi simba vita hakujilimbikizia kabisa mali yule mzee japo alikuwa anamapungufu yake mengine kibinaadamu! alikataa katakata yule mzee kujengewa majumba ya kifahali japo aliwahi kushika vyeo mbalimbali serikalini likiwamo lakuwa makamu wa rais wakwanza wa Tanzania,leo hii gavana ana jenga jumba la pesa yote ile hebu jiulizeni nyie mnao jiita wabongo wakileo uzalendo wenu uko wapi wajameni?
halafu mnaenda kumuaga mzee wawa watu eti nanyie mnajiita wanafunzi wake angekuwa na uwezo wakunyanyuka ange watandika bakora za mbavu!
Enter your comment below:
Your Name:

Your Comment:


Enter the security code below
ntr8

Tanzania kuipiku Marekani kwa Uranium
Denmark will be dependent on immigrants
helikopta za kukodi zatua dar
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
The Danish public accounts committee gets a close look at Danish support in Tanzania
Australian magistrate rules that the 'N-word' is not offensive
New rules regarding residence permits for au pairs
Muhidin Michuzi: Libeneke jipya - michuzipost.com
Denmark Starts to Trim Its Admired Safety Net
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
Danish Immigration Service: Information about law changes
Youth-to-youth fund launched in Tanzania and Uganda
DF: People with non-Western background are not welcome in DK
Zimbabwe yataka mabalozi wa nchi za magharibi kuomba msamaha
Denmark : PM rejects DF demands on immigration
Mzungu Kichaa - new judge for Tanzania TV talent show , bongo star search
Vigogo waanguka uchaguzi wabunge CCM. Malecela nje!
Colonialism and the 'scramble for Africa'
Untold story: Night meeting that saved Moi presidency
Mdanish Jan Poulsen atua Tanzania kumrithi Maximo
Zanzibar votes for unity gov't
Family reunification with a foreign spouse: 24-years rule update
Tanzania traveler shares beauty of arrival
Banking executive: wages are too high
Copenhagen: Bilinguals feel like second rate students
Tanzania: Local Govts Frustrating Country Revenues
Au pairs stay on in Denmark - as nurses
Ministry sets up ‘dating site’ for expats and Danes
Copenhagen: Police dog found DKK 5 million
Tanzania Radar Scandal: U.K. Bribery Reparations a Risky Business