Welcome to TANDEN information portal. Thursday, 9th Sep,2010
Username: Password:
Upcoming Tanzanians' events
Tomorrow - Jagwa Music Concert
11 Sep - Eid el Fitri Celebration
18 Sep - TANDEN family day
Public holidays in Denmark
24 Dec - Christmas Eve
25 Dec - Christmas Day
26 Dec - Boxing Day
Denmark: Best African Achievement Awards 2010 ■■ Press release: Mzungu Kichaa on European tour in August 2010 ■■ Dulla Mnanga Album "Nani" is out ■■ Invest in Tanzania■■ Welcome to Tanzania, the land of Kilimanjaro,Zanzibar and Serengeti
Maajabu ya Mungu ajali ya Tanga, mtoto wa miaka miwili atoka mzima
Bookmark and Share

Source : Mwananchi
Posted by: Webmaster on 03-Feb-2010

KATIKA kile kinachothibitisha maajabu ya Mungu, mtoto wa miaka miwili ametoka salama katika ajali iliyotokea juzi mkoani Tanga wakati mama yake mzazi anadaiwa kufariki dunia katika ajali hiyo.

Ajali hiyo iliyohusisha mabasi mawili ya Chatco na Nzuri, yaliyogongana uso kwa usojuzi; ilitokea eneo la Kwangahu, wilayani Handeni na kuua watu 25 na kujeruhi wengine 52.

Mtoto huyo ambaye hajaanza kuzungumza, alitoka salama katika ajali hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Bombo huku ikihofiwa kuwa mama yake ni miongoni mwa abiri waliokufa.

Mwananchi ilifika katika hospitali hiyo jana na kukuta wauguzi na waganga wakitafuta namna ya kuwapata ndugu wa mtoto huyo wa kiume ili wamchukue bila mafanikio.

Mtoto huyu ni mzima wa afya njema, kachubuka kidogo tu usoni na tumemshona alikuwa akilia kwa njaa wakati akiletwa, lakini, tulipompa chakula ameanza kucheza," alisema Fred Mtatifikolo, Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo kuongeza:

"Tumempima kuchunguza kama kuna athari alizopata mwilini tumebaini kuwa hana tatizo lolote".

Alisema tatizo alilonalo mtoto huyo ni kuwa anashangaa kuona watu wengi hospitalini hapo bila kumwona mama yake, hivyo kumfanya awe na wasiwasi mara kwa mara.

Alisema juhudi zimefanywa ili kutambua kama miongoni mwa majeruhi anaweza kuwa ni mzazi wa mtoto huyo, lakini hajapatikana.

Kwa mujibu wa mganga huyo za kumpata ndugu zimeshindikana na sasa uongozi wa hospitali hiyo imeamua kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii ambayo imeahidi kumchukua na kumpeleka katika vituo vya kulela watot yatima.

"Kama ndugu wa mtoto huyu hawatajitokeza, itabidi kumpeleka kwenye kituo cha kulea watoto yatima kitakachochaguliwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa sababu hatuwezi kumtunza hapa," alisema mganga huyo.

Kulazwa kwa mtoto huyo katika hospitali ya Bombo, kumewavuta watu wengi kutoka shemu mbalimbali, ambao waliofika katika wodi ya Galanosi kumwangalia, huku wengine wakiahidi kumlea kama wataruhusiwa.

Kuna mama amesema ataiomba Serikali imkabidhi mtoto huyo ili amlee ili iwe ni kumbukumbu ya ajali hiyo mbaya katika mwaka huu, alisema Hadija Ali mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo.

Katika hatua nyingine, jeshi la polisi lilisema ajali hiyo iliyotokea juzi imesababishwa na mwendokasi.

Ajali hiyo ilihusisha mabasi mawili ya Chatco Charter iliyotoka Dar na kwenda Arusha na basi la Nzuri aina ya Amu Mitsubishi Fusso Bus yaliyogongana uso kwa uso na kusababisha vifu vya watu 24 papo hapo52kujeruhiwa.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Simon Sirro imeeleza kuwa ajali ilitokea dereva wa Chatco akiwa mwenye mwendo wa kasi akijaribu kulipita lori ambalo bila tahadhari na kusababisha kugongana uso kwa uso na basi la Nzuri ambalo dereva wake alifariki dunia papo hapo.

Taarifa ilisema dereva wa basi la Chatco alijisalimisha polisi jana.

Taarifa hiyo imefahamisha kuwa idadi ya watu waliokufa katika ajali hiyo imeongezeka baada ya watu wawili zaidi waliokuwa wamekimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Korogwe,Magunga kwa ajili ya matibabu kufariki dunia wakipatiwa matibabu.

Wakati wagonjwa wengine wakiendelea na matibabu hospitalini hapo, miili ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo na kupelekwa katika hospitali ya Bombo imeanza kuchukuliwa na ndugu zao.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Fredy Mtatifikolo alisema hadi jana mchana maiti 13 walidhatambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao.

Waliotambuliwa ni Hamida Ibrahim Mwanga (50), wa Same, utingo wa basi la Chatco, Abdallah Hassan Mvungi (24) wa Lembeni, Mwanga, Upendo Omari wa Kihurio Jitengeni, Same; Bakari Abdallah Jambia (40) wa Dar es Salaam na Zuberi Semkiwa (30) wa Korogwe na ambaye ni kondakta.

Wengine ni Major John Malimi Holela (43) wa JWTZ mkazi wa Buguruni, Dar; Vera Kinabo (41) mfanyabiashara wa Arusha, Mickidadi Senkondo (60) mfanyabiashara wa Sinza, Dar; Urban Tambo Hiacent (33), fundi umeme kutoka Kimara, Dar na Sultan Yahya Sultan (41) wa Manzese Uzuri Dar.

Majeruhi ni ni Erasto Josnail Mmanga (30) wa Kahe, Moshi, Ramadhani Suma Msuya (65) wa Lushoto, Sadi Saidi (19) wa Bungu Korogwe, Ramadhani Athumani (30) wa Lembeni, Hamisi Bakari (26) wa Goba, Dar; Mashanga Omari (28) wa Kimara, Dar na Theresia Mangia (47) wa Mbezi, Dar.

Wengine ni Buhairu Hashimu (18) mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bungu, Rahimu Hashim (12) mwanafunzi wa Bungu, Korogwe; John Emmanuel Lukumai (45) wa Kerenge Bagamoyo, Nuru Samasimba (70) wa Komkonga, Handeni, David Kiswaga (25) wa Tandale, Dar; Sara Ali (25) wa Ubungo, Dar na Abdallah Mateyanga

(32) wa Manzese, Dar.

Wengine ni Kassim Saidi (43) wa Kibaha, Pwani, Frank Thomas (20), wa Kirua Vunjo, Moshi; Halfani Ramadhani (35) wa Mnazi, Lushoto; Daudi Lyakito (27) wa Kariakoo, Dar; Ramadhani Omari (40), wa Dar; Anuari Ramadhani (6) wa Dar es Salaam, Bonaventure Simon Kiara (36) wa Kirima Kibosho, Moshi;Lekey Jesse Giliad (55) wa Old Moshi; Asha Mohamed (32) wa Tabata, Dar na Hassan Ramadhani (35) wa Mnazi, Lushoto.

Watu wengine waliojeruhiwa ni Ravina Bea (23) wa Mponde Tea Estate, Lushoto, Jackson Adama (16), mwanafunzi wa Suji Secondary School, Nivew Amos (27) Mbagala, Dar, Samwel Ibrahim Nko (29), wa Babati, Manyara, Erick Richard (37) wa Tabata, Dar, Godfrey Prosper (27) wa Moshi, Major Kassim Chambo wa Kibaha, Eliunura Mosha (47) wa Dar, Mary Emily (26) wa Lushoto, Hadija Selemani (4) wa Tabata na Lucy Andrea (25) wa Hedaru.

Majeruhi wengine ni Mariam Joseph (45) wa Mwananyamala Kisiwani, Dar; Mwajuma Mohamed (60) wa Komkonga, Handeni; Sakimea Togolai (35) wa Kwadole, Lushoto; Sindo Alban Sindo (dereva wa Nzuri Trans); Yassin Ayoub (25) wa Moshi, Mohamed Salimu (18) na Bashiru Issa (21) wote wakiwa wanafunzi wa Soweto, Moshi; Elizabeth Simon (49) wa Kerenge, Bagamoyo; Hadija Chambo (18) wa Masatu, Korogwe na mwingine ambaye alitambuliwa kwa jina la Zaina (9). Jenifa Ngama (36) wa Mwanga na Hadija Hamisi (25) wa Korogwe. Abiria watatu ambao ni mahututi bado hawajatambuliwa.

Enter your comment below:
Your Name:

Your Comment:


Enter the security code below
6j4q

Tanzania kuipiku Marekani kwa Uranium
Denmark will be dependent on immigrants
helikopta za kukodi zatua dar
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
The Danish public accounts committee gets a close look at Danish support in Tanzania
Australian magistrate rules that the 'N-word' is not offensive
New rules regarding residence permits for au pairs
Muhidin Michuzi: Libeneke jipya - michuzipost.com
Denmark Starts to Trim Its Admired Safety Net
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
Danish Immigration Service: Information about law changes
Youth-to-youth fund launched in Tanzania and Uganda
DF: People with non-Western background are not welcome in DK
Zimbabwe yataka mabalozi wa nchi za magharibi kuomba msamaha
Denmark : PM rejects DF demands on immigration
Mzungu Kichaa - new judge for Tanzania TV talent show , bongo star search
Vigogo waanguka uchaguzi wabunge CCM. Malecela nje!
Colonialism and the 'scramble for Africa'
Untold story: Night meeting that saved Moi presidency
Mdanish Jan Poulsen atua Tanzania kumrithi Maximo
Zanzibar votes for unity gov't
Family reunification with a foreign spouse: 24-years rule update
Tanzania traveler shares beauty of arrival
Banking executive: wages are too high
Copenhagen: Bilinguals feel like second rate students
Tanzania: Local Govts Frustrating Country Revenues
Au pairs stay on in Denmark - as nurses
Ministry sets up dating site for expats and Danes
Copenhagen: Police dog found DKK 5 million
Tanzania Radar Scandal: U.K. Bribery Reparations a Risky Business