Welcome to TANDEN information portal. Thursday, 9th Sep,2010
Username: Password:
Upcoming Tanzanians' events
Tomorrow - Jagwa Music Concert
11 Sep - Eid el Fitri Celebration
18 Sep - TANDEN family day
Public holidays in Denmark
24 Dec - Christmas Eve
25 Dec - Christmas Day
26 Dec - Boxing Day
Denmark: Best African Achievement Awards 2010 ■■ Press release: Mzungu Kichaa on European tour in August 2010 ■■ Dulla Mnanga Album "Nani" is out ■■ Invest in Tanzania■■ Welcome to Tanzania, the land of Kilimanjaro,Zanzibar and Serengeti
Mtanzania aliyeuawa India azikwa bila kichwa
Bookmark and Share

Source : Tanzania Daima
Posted by: Webmaster on 07-Feb-2010

VILIO, simanzi na majonzi jana vilitawala mazishi ya Mtanzania Imran Mtui (31) aliyeuawa kikatili nchini India hivi karibuni, katika mazishi yaliyofanyika makaburi ya Njoro Manispaa ya Moshi.
Hata hivyo mwili huo ulizikwa bila kichwa huku pia ukidaiwa kuwa na majeraha mengi mwilini kuanzia miguuni na kwenye paja lake karibu na kiuno huku kiwiko cha mkono wa kulia nacho kikidaiwa kunyofolewa.

Mwili huo uliwasili mjini moshi usiku wa kuamkia jana baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es salaam, ukitokea nchini India huku gharama zote za kuusafirisha zikibebwa na serikali ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kabla ya mazishi, kaka wa marehemu, Maliki Mtui, alisema kuwa wameshtushwa na kifo cha ndugu yao hasa kutokana na marehemu kutokuwa na historia ya ugomvi.

Kwa mujibu wa kaka huyo, mwili huo pia umeonekana kuwa na alama za kamba kwenye mikono yake hali ambayo inaonyesha marehemu kabla ya kuuawa alifungwa kamba ili asiweze kujitetea.

Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kutokea katika mji wa Bangalore nchini India ambako marehemu alikuwa tayari amehitimu masomo yake ya biashara na utawala (Business Administration) na tayari alikuwa akijiandaa kurejea nyumbani.

Kaka huyo wa marehemu aliwaambia waandishi wa habari kuwa mdogo wake huyo alipatwa na mkasa huo akiwa njiani kuelekea mjini ambako rafiki yake wa kike ambaye pia ni Mtanzania aishie visiwani Zanzibar alikuwa akisoma.

“Niliwasiliana naye siku ya tukio kabla hajapatwa na mauti haya nikamuuliza anatarajia kurudi lini nyumbani akanijibu angerudi mapema na rafiki yake alikuwa akimsubiri lakini hakuweza kutokea” alisema.

Pamoja na kuishukuru serikali ya Tanzania kugharamia kuusafirisha mwili wa marehemu mdogo wake, Mtui ameitaka pia serikali kuwathamini raia wake walioko nje ya nchi kwa kufuatilia taarifa zao pindi wanapokumbwa na matukio kama hayo ya kuuawa kwa mdogo wake.

Naye msemaji wa familia ya marehemu Mtui ambaye pia ni shekhe wa msikiti wa Majengo, Shekhe Said Khatibu alisema kuwa serikali haiwathamini raia wake walioko nje na ndiyo maana serikali haijatoa tamko rasmi kulaani mauaji hayo.

Shekhe huyo pia alisema katika kile kinachoonyesha kuwa idara za serikali zimelala, serikali imeshindwa kutuma hata mwakilishi kwenye mazishi hayo ambayo tukio lake lina utata.

Aidha, alipinga taarifa zote zilizotolewa na madaktari nchini India kwamba marehemu alifariki dunia kwa ajali ya treni na kusisitiza kuwa taarifa hizo sio za kweli.


Comments
On 7th Feb,2010 Dunia wrote
What a shame! What great loss of life!
On 9th Feb,2010 mtanzania denmark wrote
Hilo ni jambo la kusikitiza sana kunzikwa bila kichwa? lakini tunamuombea ndugu yetumngu amuweke peponi hata bila kichwa
Enter your comment below:
Your Name:

Your Comment:


Enter the security code below
y6r7

Tanzania kuipiku Marekani kwa Uranium
Denmark will be dependent on immigrants
helikopta za kukodi zatua dar
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
The Danish public accounts committee gets a close look at Danish support in Tanzania
Australian magistrate rules that the 'N-word' is not offensive
New rules regarding residence permits for au pairs
Muhidin Michuzi: Libeneke jipya - michuzipost.com
Denmark Starts to Trim Its Admired Safety Net
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
Danish Immigration Service: Information about law changes
Youth-to-youth fund launched in Tanzania and Uganda
DF: People with non-Western background are not welcome in DK
Zimbabwe yataka mabalozi wa nchi za magharibi kuomba msamaha
Denmark : PM rejects DF demands on immigration
Mzungu Kichaa - new judge for Tanzania TV talent show , bongo star search
Vigogo waanguka uchaguzi wabunge CCM. Malecela nje!
Colonialism and the 'scramble for Africa'
Untold story: Night meeting that saved Moi presidency
Mdanish Jan Poulsen atua Tanzania kumrithi Maximo
Zanzibar votes for unity gov't
Family reunification with a foreign spouse: 24-years rule update
Tanzania traveler shares beauty of arrival
Banking executive: wages are too high
Copenhagen: Bilinguals feel like second rate students
Tanzania: Local Govts Frustrating Country Revenues
Au pairs stay on in Denmark - as nurses
Ministry sets up ‘dating site’ for expats and Danes
Copenhagen: Police dog found DKK 5 million
Tanzania Radar Scandal: U.K. Bribery Reparations a Risky Business