Welcome to TANDEN information portal. Thursday, 9th Sep,2010
Username: Password:
Upcoming Tanzanians' events
Tomorrow - Jagwa Music Concert
11 Sep - Eid el Fitri Celebration
18 Sep - TANDEN family day
Public holidays in Denmark
24 Dec - Christmas Eve
25 Dec - Christmas Day
26 Dec - Boxing Day
Denmark: Best African Achievement Awards 2010 ■■ Press release: Mzungu Kichaa on European tour in August 2010 ■■ Dulla Mnanga Album "Nani" is out ■■ Invest in Tanzania■■ Welcome to Tanzania, the land of Kilimanjaro,Zanzibar and Serengeti
Watu 46 wanusurika ajali ndege ya ATCL
Bookmark and Share

Source : Ippmedia
Posted by: Webmaster on 02-Mar-2010

Abiria 39 pamoja na wafanyakazi saba waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la ATCL aina ya Boeing 737 kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza jana walinusurika kufa baada ya ndege hiyo kuacha njia wakati ikitua katika uwanja wa ndege jijini Mwanza.

Kumekuwa na habari za kutatanisha juu ya chanzo cha ajali hiyo, huko baadhi ya vyanzo vya habari vikisema ni kuzima kwa injini, vingine ni kupasuka kwa tairi ya mbele ilhali vingine vikisema ni hali mbaya ya hewa.

Habari za kiuchunguzi zilizofanywa na mwandishi wetu jijini Mwanza zinasema kwamba wakati ndege hiyo ikitua tairi zake za mbele zilipata pancha na kuifanya kuacha njia huku bawa lake moja likiwa limebakia kwenye njia ya kutua.

Habari hizo zinasema kwamba ndege ikiwa tayari imekwisha kushika njia ya kutua, iliserereka umbali wa mita kadhaa na kuingia katika matope huku bawa lake moja likibaki kwenye njia.

Kamanda wa zimamoto kanda ya Ziwa, Juma Kwiyamba, alisema ndege hiyo yenye usajili namba 5H-MVZ ilipata ajali kati ya saa 1.40 na 1.45 asubuhi.

Kamanda huyo alisema chanzo cha ajali hiyo inawezekana kuwa ni hali ya hewa kwani wakati inatokea kulikuwa na mvua kubwa, ukungu pamoja na upepo mkali.

Naye Kaimu Meneja wa uwanja wa ndege wa jijini Mwanza, Byantao Muchunguzi, alisema kuwa wakati ndege hiyo ikitua tairi za mbele ziling’oka na hivyo kusababisha kuyumba na kwenda kwenye matope.

“Tunashukuru Mungu hakuna abiria aliyejeruhiwa, wote wametoka salama ila ni mishtuko midogo midogo,” alisema Muchunguzi.

Muchunguzi alisema kufuatia ajali hiyo uwanja huo umefungwa kwa muda usiojulikana hadi ndege hiyo itakapofanyiwa matengenezo na kuondoka.

Alisema kwa sasa wanasubiri wataalam kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha ajali hiyo pamoja na kuifanyia matengenezo.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonosius Komba, alisema wakati ndege hiyo ikitua uwanja ulikuwa umejaa maji hivyo kusababisha injini moja ya kulia kuzima.

Alifanunua kuwa baada ya injini kuzima ndege ilianza kuvutwa upande mmoja umbali wa mita 400 hadi kusimama.

Alisema ndege hiyo ilikuwa ikirushwa na rubani Joseph Ibanda akisaidiwa na rubani aliyejulikana kwa jina moja la Mwakang’ata.

Hali kadhalika, Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usalama wa Anga (TCAA), Abel Ngapemba, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Ngapemba alifafanua kuwa ajali hiyo ilisababishwa na tairi za mbele kung’oka hali iliyosababisha ndege hiyo iyumbe na kunasa kwenye matope.

Mwishoni mwa wiki iliyopita ndege ya shirika hilo ilishindwa kutua na kulazimika kwenda uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha jijini Mwanza.

Wakati huo huo, abiria zaidi ya 120 waliokuwa wasafiri na shirika la ndege la Precision wamekwama kusafiri kutokana na uwanja wa ndege kufungwa kwa muda usiojulikana.

Kwa mujibu wa Ofisa Mauzo wa Shirika hilo, Hillary Edward, wengi wa abiria walikuwa wasafiri na Boeing kwenda jijini Dar es Salaam jana mchana.

“Tumelazimika kusitisha safari za ndege mbili baada ya uwanja kufungwa. Hata hivyo bado tunawasikiliza watalaamu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kujua uwanja utafunguliwa lini,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

Enter your comment below:
Your Name:

Your Comment:


Enter the security code below
46gy

Tanzania kuipiku Marekani kwa Uranium
Denmark will be dependent on immigrants
helikopta za kukodi zatua dar
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
The Danish public accounts committee gets a close look at Danish support in Tanzania
Australian magistrate rules that the 'N-word' is not offensive
New rules regarding residence permits for au pairs
Muhidin Michuzi: Libeneke jipya - michuzipost.com
Denmark Starts to Trim Its Admired Safety Net
Jobsearch Kick-Off Course on September 14
Danish Immigration Service: Information about law changes
Youth-to-youth fund launched in Tanzania and Uganda
DF: People with non-Western background are not welcome in DK
Zimbabwe yataka mabalozi wa nchi za magharibi kuomba msamaha
Denmark : PM rejects DF demands on immigration
Mzungu Kichaa - new judge for Tanzania TV talent show , bongo star search
Vigogo waanguka uchaguzi wabunge CCM. Malecela nje!
Colonialism and the 'scramble for Africa'
Untold story: Night meeting that saved Moi presidency
Mdanish Jan Poulsen atua Tanzania kumrithi Maximo
Zanzibar votes for unity gov't
Family reunification with a foreign spouse: 24-years rule update
Tanzania traveler shares beauty of arrival
Banking executive: wages are too high
Copenhagen: Bilinguals feel like second rate students
Tanzania: Local Govts Frustrating Country Revenues
Au pairs stay on in Denmark - as nurses
Ministry sets up ‘dating site’ for expats and Danes
Copenhagen: Police dog found DKK 5 million
Tanzania Radar Scandal: U.K. Bribery Reparations a Risky Business