Posted by: Webmaster on 10-Mar-2010
Tunapenda kuwataarifu kuwa limepatikana darasa kwa ajili ya kufundishia lugha ya kiswahili kwa watoto wa wanachama,wake, waume, ndugu, watanzania wote na wale ambao wangependa kujifunza lugha ya kiswahili.
Tunawaomba wale ambao wanapenda kushiriki au watoto wao, waweze kujiandikisha kwa kutuma e-mail kwa katibu wa Tanden. katibu@watanzania.dk
Darasa litakuwa siku za weekend jumamosi, hii imezingatia kuwa washiriki wataweza pia kufanya shughuli zao kama kawaida siku za wiki. Watu wazima watafundishwa tofauti na watoto(kwa mda tofauti na hawatachanganywa darasa moja na watoto) hivyo msihofu kujiandikisha.
Mwisho wa kujiandikisha ni tarehe 15.04.2010. Siku ya alhamisi saa 12 jioni. Tunaomba uonapo tangazo hili umtaarifu na mwenzako.
By Uongozi Tanden.
| On 9th Apr,2010 Sawa wrote |
| Hayo ni maendeleo au vipi? Tuchangamkia basi??? |

