Posted by: Nikita on 19-Jul-2010

Mechi ya kwanza kati ya Tanden fc na Parken fc iliyofanyika jumamosi 17/7/2010,ilimalizika kwa mabao 4 zidi ya 6 kwa Parken fc.
Ilikuwa ni zoezi tosha kwa Tanden fc, ambayo ndiyo ilikuwa mechi ya kwanza tangu Tanden mpya,yenye mtazamo mpya(kwa pamoja tutafika)kuanzishwa.
Tunawapongeza tena kwa watanzania waliojitokeza ,kushuhudia mpambano huo, kwani pia ilitia motisha kwa wachezaji kujituma.Ukizingatia timu ya parken inafanya mazoezi mara tatu kwa wiki!.
Pongezi nyingine ziwaendee wachezaji wote waliofika siku ya jumamosi,Tanden fc bado inaendelea kutoa wito kwa watanzania wote waishio Denmark,wanakaribishwa kwa moyo mkunjufu kwaajili ya kuchangamana,kujuana na kufurahi kwa pamoja katika kucheza mpira wa miguu.
Kutakuwa na mazoezi tena jumamosi ijayo ya tarehe 24/7/2010 saa saba mchana, nyote mnakaribishwa.

