Warning: Trying to access array offset on value of type bool in /customers/c/7/7/watanzania.dk/httpd.www/wp-content/themes/diplomat/helper/helper.php on line 256

TANZIA TANZIA TANZIA

TANZIA TANZIA TANZIA

UPDATES ZA MAREHEMU SAMUEL JOHN ASHELI:
Kwa habari tulizopata hivi punde, ndugu wa marehemu Samuel  John Asheli wamepatikana huko Nyumbani (Tanzania ) na mipango ya kukutana wana ndugu inaanza kufanywa ili kuona namna gani wanaweza kushiriki kwenye mazishi ya Samuel hapa Denmark au kumpeleka Tanzania.

Tunashukuru nyote mlioweza fanikisha kwa njia moja ama nyingine kwa habari kusambazwa hadi kufikiwa walengwa.

"UMOJA NI NGUVU"

Screen Shot 2016-08-10 at 22.47.35

Ndugu wanachama na marafiki wa TANDEN.

Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli aka Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +4561283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze  kuhudhuria mazishi yake.

 

DM_WatanzaniaDK

Related Articles

Close
Close

Please enter your username or email address. You will receive a link to create a new password via email.

Close

Close