Tunaweza kutimiza malengo yetu

Tunaweza kutimiza malengo yetu

Tunaweza kutimiza malengo yetu

Katika jitihada za kuleta maendeleo Tanzania, vyama vya watanzania waishio nje ya Tanzania ama waTanzania waishio nje ya Tanzania "Diaspora" wanakila sababu ya kuungana na kufanya mambo makubwa katika nchi yetu ya Tanzania, kwenye nyanja mbalimbali ( Afya,Kilimo,Biashara na Elimu)

Dhana hii haiwezi kufikiwa kwa upana kama hamana umoja na ushirikiano katika vyama (vikundi) vetu vilivyopo nje ya Tanzania.katika kudumisha ushirikiano huu ni lazima wana Diaspora wajaliane,washirikiane na kua hai katika vyama vyao ili kusudi malengo ama lengo la vyama vyao viweze kutimia.

Kwa mfano TANDEN inamalengo mazuri tu ya kutaka kusaidia na kama inavyoendelea kusaidia katika nyanja mbalimbali nyumbani, lakini ikiweza kupata ushirikiano mzuri kwa watanzania wanaishi hapa Denmark zaidi ya wanao upata sasa. Nafikiri TANDEN inaweza kua mfano wa kuigwa kwa wanaDiaspora wengine duniani na lile swali la sababu  1000 za kuwashirikisha wanadiaspora katika ujenzi wa Taifa inaweza kua rahisi na kua mara tatu au nne ya 1000.

26804799_2234318183252527_6021426630421263993_n jiko1149660346293010300_resized

waikato wa msosi

Kutokana na na ule usemi wa wahenga ya kwamba "umoja ni nguvu" kwa wana Tanden "Diaspora" inabidi tuupigilie msumari kwenye vinwa na akili zetu ili tuweze timiza malengo ya Tanden na pia kusaidia katika kujenga uchumi wa Tanzania kwa watoto na wajukuu zetu. Kumbuka ya kwamba mji wa Rome haukujengwa kwa siku moja bali ilichukua siku,miezi,miaka na karne mpaka kuja kuimarika.

kwa maantiki hayo basi Tanden inawahusia wanachama wake na watu wote waipendayo nchi ya Tanzania hususani wanaoishi Denmark kufanya yafuatayo

  1. Kulipia ada ya mwaka 100kr kwa kupitia Danske Bank Reg No:4120 Account no: 4120026739
  2. Kushiriki katika vikao vya kamati na mkutano mkuu
  3. kushiriki katika hafla na matukio mbalimbali ya Tanden
  4. Kuitangaza Tanzania kwa wadau mbalimbali

Tukiweza fanya hivi basi hakuna sababu yoyote ambayo itakwamisha uwezo wa sisi wanadiaspora kutekeleza wajibu wetu wa kulijenga Taifa letu la Tanzania, kwa vizazi vinavyokuja na kudumisha ushirikiano wetu hapa Denmakr kwa hali na mali.

"Umoja ni nguvu" iwe ndio kauli mbiu yetu.

Habari hii imeandikwa katika kuamsha na kuchangia hoja ya nakala kutoka kwenye gazeti la mwanachi katika masuala ya diaspora Sababu 1000 za diaspora za kuwashirikisha katika ujenzi wa Taifa.

DM_WatanzaniaDK

Related Articles

Close
Close

Please enter your username or email address. You will receive a link to create a new password via email.

Close

Close