mTanzania apata medali ya shaba Aarhus

mTanzania apata medali ya shaba Aarhus

mTanzania apata medali ya shaba Aarhus

Mtanzania  apata medali ya shaba katika mchezo wa kutupa mkuki:

mTanzania Shururwai Laanyuni  amepata ushindi wa kutupa mkuki kwa wanaume miaka 60 - 64 kwenye mashindano ya Ulaya mzima katika mji wa  Aarhus. 

#watanzaniadk #emacs2017 #michezodk #emacs #chamachawatanzaniadenmark

Amekuwa mshindi wa tatu katika kutupa mkuki kwa wenye umri wa miaka 60 - 64 katika mashindano ya watu kuanzia umri wa miaka 35 kwenda juu kwa nchi zote za Ulaya EMACS (European Masters Athletics Championships Stadia).

IMG_5934 (Bofya hapo kuona video yake akirusha mkuki)

Michezo hii hufanyika kila baada ya miaka miwili.

Mara ya kwanza na mwisho kushiriki Shururwai Laanyuni ilikuwa mwaka 2004 kwenye mkuki; na kufanikiwa kushika nafasi ya 6.

Mwaka huu amebahatika kupata nafasi ya tatu, na kupata medali ya shaba (bronze).

Kwa ushindi wake huo pia unatufundisha kwamba hata sisi waTanzania tuishio ughaibuni hususani hapa Denmark tunayo nafasi ya kuungana pamoja na kufanya michezo kama familia, kwani michezo ni afya na pia hukutanisha wana jamii ya watanzania na wazawa wa hapa Denmark.

DM_WatanzaniaDK

Related Articles

The Copenhagen Revival Conference

Close
Close

Please enter your username or email address. You will receive a link to create a new password via email.

Close

Close